Sunday, 8 January 2017

BURIANI RAIS WA USHELISHELI


Rais wa kwanza wa Ushelisheli, taifa lililoko katika kisiwa kilicho kwenye Bahari Hindi, James Mancham, amefariki.

Mancham amefariki akiwa na umri wa miaka 77.

Inaripotiwa kuwa alipatikana na wafanyikazi wake akiwa amezirai ndani ya nyumba.

Wakili wake Sir James, baadaye alichukua hatamu ya Urais mnamo mwaka 1976 baada ya kushinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa kwanza nchini humo.

Ushelisheli zamani ilitawaliwa na Uingereza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive