Saturday, 14 January 2017

OMOG ALIKUBALI GOLI LA HIMID


Ule ‘muwa’ uliopigwa na Himid Mao kuiandikia bao Azam dakika ya 13 kipindi cha kwanza hakua wa mchezo-mchezo kabisa.
Himid aliachia kombora kali ambalo golikipa wa Simba Daniel Agyey hakujua lilipita wapi kwenda nyuma ya nyavu zake.
Baada ya mechi kumalizika, Himid alikwenda kusalimiana na kocha wa Simba Joseph Omog ambaye alimfundisha kiungo huyu wakati walipokuwa pamoja Azam kabla ya Omog kutimuliwa ndani ya klabu hiyo.
Omog hakuacha kumpongeza Himid kwa aina ya goli aliloifunga Simba na kuipa Azam ubingwa wa tatu wa Mapinduzi Cup katika historia.
“Congratulations, it is a fantastic goal,” anasema Omog akionesha kulikubali bao la Himid ambaye aliwahi kumfundisha wakati alipokuwa kocha mkuu Azam FC na kufanikiwa kushinda taji la VPL mara ya kwanza msimu wa 2013-14.
Goli la Himid Mao lilikuwa la saba kwa Azam kwenye mashindano ya mwaka 2017 huku yenyewe ikiwa haijaruhusu goli hata moja hadi mwisho wa mashindano.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive