Michuano ya 31 ya kombe la mataifa Bingwa Afrika, inatarajiwa
kuanza jumamosi January 2017 wenyeji Gabon watakapokabiliana na
Guinea-Bissau ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
AFCON kwa sasa ni michuano yenye ushindani mkali na yenye wachezaji
nyota kama vile Riyad Mahrez, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang.
Wakati michuano hii inapong’oa nanga, BBC wameyaweka matukio muhimu ya
kukumbukwa ambapo yapo yanayofurahisha na ya kusikitisha pia ambayo
hayatasahauliki katika historia ya AFCON.
1994: Timu ya Zambia baada ya kupata ajali ya ndege ilijijenga na kuingia fainali AFCON
April 27 1993, timu ya taifa ya Zambia ilikuwa safarini mechi ya
kufuzu Kombe la Dunia nchini Senegal ndege iliyowabeba ilipoanguka na
kutumbukia baharini mita 500 kutoka mji wa Libreville, Gabon.
Abiria wote 25 walikufa pamoja na wahudumu watano. Mwaka mmoja
baadaye, Zambia ilijijenga upya na michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa
Afrika 1994 walifika fainali ingawa walishindwa na Nigeria 2-1.
2012: Herve Renard asaidia Zambia kutwaa kombe
Zambia walikosa ushindi fainali 1994 lakini walifanikiwa 2012 chini
ya kocha wao Mfaransa Herve Renard ambapo walikabiliana na Ivory Coast
fainali. Kwenye mechi hiyo, Zambia ilishinda kwa penalti 8-7.
2015: Morocco yajiondoa kwa sababu ya Ebola
Kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, wenyeji
waliopangiwa kuandaa michuano ya 2015 Morocco walijiondoa wakihofia
michuano hiyo ingefikisha ugonjwa huo nchini mwao.
CAF ilikataa ombi la kujiondoa na baada ya Morocco kusisitiza timu
yake ikafurushwa kutoka kwa michuano hiyo. Mataifa matano yalikataa kuwa
mwenyeji kabla ya Equatorial Guinea kukubali. Ivory Coast waliibuka
washindi kwa penalti 9-8 dhidi ya ghana.
2010: Basi la Togo lashambuliwa
Basi la timu ya Togo lilishambuliwa na watu wenye silaha timu hiyo
ilipokuwa ikirejea kambini Angola. Kundi moja la waasi kutoka eneo la
Cabinda lilikiri kuhusika
Watu watatu waliuawa na wengine tisa kujeruhiwa. Nyota wa zamani wa
Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor ni miongoni mwa waliokuwa
kwenye basi hilo. Togo ilijiondoa kutoka kwa michuano hiyo.
2006 & 2012: Drogba alivyotumia nafasi yake kufanikisha amani nchini kwake.
Wakati wa vita kati ya 2002 na 2007 mshambuliaji wa Ivory Coast
Didier Drogba alitumia nafasi yake kufanikisha amani nchini kwake,
alipiga magoti moja kwa moja kwenye akiwa na wachezaji wenzake
kuwahimiza waliokuwa wanapigana kuweka chini silaha.
Kipindi cha amani kilifuata, mwaka 2008, alisisitiza mechi ya kufuzu
Kombe la Taifa Bingwa Afrika dhidi ya Madagascar ichezewe ngome ya
zamani ya waasi Bouake kama wito kwa raia kuungana.
Mwaka 2006 na 2012, Drogba alisaidia taifa lake kufika fainali za
Kombe la Mataifa Bingwa Afrika lakini wakashindwa kwa mikwaju ya penalti
hata hivyo, hakufanikiwa kushinda.
2002 & 2004: Jezi za Cameroon
Cameroon walishinda michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2002
kwa kulaza Senegal kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali lakini
kinachokumbukwa sana ni jezi za Simba Wasioshindwa ambazo zilikuwa
hazina mikono. FIFA hata hivyo waliwazuia kuziva wakati wa Kombe la
Dunia 2002.
Mwaka 2004 walikuwa na mpya tena baada ya kuvalia jezi moja
iliyoshikana fulana na kaptura nchini Tunisia. FIFA hawakufurahia na
ikizingatiwa kwamba walikiuka ahadi ya awali ya kuzitumia kucheza mechi
za makundi pekee, FIFA waliwapiga faini kwa kucheza mechi ya robo
fainali ambayo walishindwa na Nigeria.
0 comments:
Post a Comment