Kama
unakumbuka mwishoni mwa mwaka 2016, raia na wafuasi wa vyama vya
upinzani nchini Zimbabwe waliandamana kupinga utawala wa Rais Robert
Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu 1980.
Habari
zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa zimedai kuwa maafisa
wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri
kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.
Pasta Patrick Mugadza alikamatwa akiwa
mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi
nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi amewambia waandishi wa
habari kuwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa
Wakili wake ameimbia AFP kuwa …….>>>‘Alikuwa
amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa
mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo’
‘Awali alishtakiwa kwa kukosea
heshima mamlaka ya Rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na
kuwa amewatusi watu wa asili fulani au dini fulani’.
Pastor Mugadza wiki iliyopita aliandaa kikao na wanahabari ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktober 17 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment