Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Dar es Salaam Young Africans, leo January 5 2017 ameandika barua kwenda kwa shirikisho la soka Tanzania TFF kuomba kupunguziwa adhabu yake aliyofungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.
Jerry Muro alifungiwa
na kamati ya maadili July 7 2016 kwa makosa mawili, moja alilifanya
mwaka 2015 la kukaidi kulipa faini ya Tsh milioni 5 iliyoamuliwa kulipa
na kamati ya nidhamu baada ya kufanya makosa na ndio kosa ambalo
limemfanya afungiwe mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh
Milioni 3.
0 comments:
Post a Comment