Friday 30 December 2016

NIKKI MBISHI AFUNGUKA KUHUSU HALI CHID BENZI



Leo December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika kuhusu hali ya rapa anayetawa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid.

Nikki Mbish amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye.
Unaweza kusoma kila kitu alichokiandika hapa chini kupitia Instagram.

“Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni #FEDHEHA tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya #CHID_BENZ haiko tayari kusaidiwa kuacha #NGADA.  Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya #LAWAMA na kujiona anaonewa ili hali ana #HAKI sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa.

Kuna waathirika wengi wa madawa ya kulevya hawajawahi hata kujaliwa kwa kupata hata msaada wa kupelekwa #REHAB lakini Chid alishikwa mpaka na vitu Airport na yakasawazishwa.  Je,angeshikwa mtu mwingine si ndo ingekuwa n’tolee? He took it for granted, he is ungrateful… Wasaidizi wamechoka pia.  #NINI_KIFANYIKE na yeye hayuko tayari? – Nikki Mbishi
nikki-mbish
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive