MOJA kati ya usajili ulioshangaza washabiki wa soka ulimwenguni ni ule wa Zlatan Ibrahimovic baada ya kusajiliwa na Manchester United akitokea Paris saint German ya Ufaransa.
Ambapo mchezaji huyo wenye utaifa wa Sweden alisajili katika kipindi cha dirisha dogo akitokea paris Saint German ya nchini Ufaransa.
Wengi hawakutegemea kuona Zlatan akifanya vizuri na Man United
kutokana na umri wake halafu alikuwa anaingia Ligi mpya, hivyo
iliaminika kuwa angeweza kuchelewa kufanya vizuri au kushindwa kabisa, ila Zlatan amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Man United na leo anaweza kuvunja rekodi ya Lionel Messi.
Zlatan anaweza kuvunja rekodi ya Messi kwa kufunga magoli 51 kwa mwaka 2016 kabla mwaka haujaisha, kwani Zlatan kafunga magoli 50 kwa mwaka 2016 kama akifunga goli mbili katika mchezo wa leo dhidi ya Middlesbrough anaweza kuvunja rekodi ya Messi kwa kufikisha magoli 52 wakati huu ambao Ligi ya Hispania imesimama.
0 comments:
Post a Comment