Home »
KILIMO
» HATIMAE MBEGU ZA NGANO KUANZA KUTENGENEZWA MAABARA KWA KEMIKALI MAALUMU
Kama
huli maandazi basi utakula chapati, mkate, keki ama katika vinywaji
vyenye kilevi kama bia ambavyo vyote hivi hutegemea mmea wa ngano.
Watafiti wa Uingereza wametoa makala kwenye gazeti la Maumbile wakisema
wamegundua njia mpya ya kuinua uzalishaji wa ngano kwa asilimia 20
katika maabara yao. Ngano ni chakula muhimu duniani, hivyo ugunduzi wao
huenda ukainua uwezo wa kuhakikisha usalama wa chakula duniani.
Watafiti wa Taasisi ya Rothamsted na
Chuo Kikuu cha Oxford wamezalisha kemikali tangulizi ya kemikali
nyingine iitwayo Trehalose 6 Phosphate (T6P). T6P ni kemikali muhimu
inayodhibiti ukuaji wa mimea.
Watafiti hao wamepanda ngano katika
maabara yao, na baada ya ngano kuchanua, walimwagilia kemikali tangulizi
kwenye ngano kila baada ya siku 5. Baada ya kuvuna, watafiti wamepima
uzito wa ngano na kiasi cha wanga na protini na kugundua kuwa ukubwa na
uzito wa ngano wote umeongezeka kwa asilimia 20.
T6P pia inaweza kuinua uwezo wa ngano
wa kukinga ukame. Watafiti hawakumwagilia maji baadhi ya ngano katika
siku 10 baada ya mbegu kuchipua na kutoa mizizi, badala yake
walimwagilia maji yenye kemikali tangulizi ya T6P katika siku ya 9,
baadaye walimwagilia maji kama kawaida na mwishowe ngano hizi bado
zilivunwa.
Watafiti wamesema kemikali tangulizi
waliyoizalisha inaweza kuichochea ngano kutoa T6P nyingi zaidi na kuleta
uzalishaji mkubwa. T6P inafanya kazi katika mimea mingi, hivyo njia hii
huenda ikatumiwa katika mazao mengi zaidi.
Dk. Matthew Paul kutoka taasisi ya
Rothamsted amesema watafiti wataendelea kufanya majaribio katika
mashamba mbalimbali ili kutafiti athari ya mazingira tofauti kwa
kemikali walizozalisha.
0 comments:
Post a Comment