Tumezoea
kuona wasanii wengi wa Tanzania wakinyakua tuzo nje ya nchi kwa kupitia nyimbo
walizoshirikishwa(collaboration) lakini hali hiyo imekuwa tofauti kabisa mwaka
huu.
Baada ya
mfalume wa Bongo fleva Alikiba kunyakua tuza nyingi za nje na ndani bila colabo
ya aina yoyote kutoka kwa msanii wa kimataifa hata wa kitaifa.
Alikiba
amenyakua tuzo mbalimbali ikiwemo ile aliyochukua mikononi mwa msanii maarufu
wa Nigeria, wizkid ambayo ni MTV EMA, katika kipengele cha Best African Act.
Wizkid
alietamba kwa kibao chake cha Oalegoba ambaye alipewa tuzo hiyo kimakosa na
hatimae ikabidi bodi ya uwandaaji wa tuzo za MTV Ema za Afrika kumuomba radha
alikiba na kumkabidhi tuzo hiyo.
Tuzo
nyingine alizochukua Alikiba ni Kenya Coast Music Awards,Celebrity Player
Awards,Afsa Award Supdates,EATV Awards 2016,Tz Insta Awards na nyinginezo
nyingi.
Alikiba
kupitia akauti yake ya Instagram alitoa pongezi zake za dhati kwa mashabiki
waliomuwezesha kunyakua tuza hizo na kudai kuwa ataendelea kunyakua tuzo nyingi
kwani anaamini uwezo anao.
“Nawashukuru
sana kwa kuniwezesha kushinda tuzo nyingi ndani ya mwaka huu am so proud of you
na nitakuwa hivyo siku zote” Alisema mfalume wa bongofleva Alikiba.
Alikiba
ambaye leo atakuwa Nairobi, nchini Kenya kwa ajili ya kupiga shoo ya funga
Mwaka alimaliza kwa kuwaribisha mashabiki wake kwenye shoo na kubainisha kuwa kama
wataweza kufika huko atafurahi sana.
0 comments:
Post a Comment