Thursday, 3 November 2016

SHABIKI ALIEMSUMBUA CHRIS BROWN ABURUZWA KOROTINI


 BY Denis Massawe
 Staa wa RNB nchini Marekani, Chris Brown alifungua  kesi mahakamani dhidi ya shabiki Danielle Patti ambaye alikua  akienda nyumbani kwake bila ruhusa ama mualiko wowote na kumsumbua.
Danielle Patti alianza kuonekana nyumbani kwa Chris tangu Desemba 2015 ambapo alikua akimtaka Chris kimapenzi na amekuwa akidai kumpenda sana hivyo anashindwa kukaa mbali naye, na hata alidai Chris ni mpenzi wake wa zamani.
chris-brown
Mahakama imeamuru shabiki huyo  akae mbali na Chris Brown na kutohudhuria show zake kwa miaka mitano ambapo sasa hivi Danielle yuko hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili na alipelekwa baada ya tukio la kuvamia nyumbani kwa Chris April mwaka huu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive