Home »
» WAKATI TANZANIA TUNAFIKIRIA MITA 100 NIGERIA WANAFIKIRIA MITA 10,000
Kichwa cha habari kinaweza
kikakuchanganya ila ukweli ni kwamba muziki wa Tanzania unasifiwa
umekuwa lakini bado wanaofanya vizuri hawafikirii kukua kimataifa zaidi,
baada ya kuliteka soka la Afrika ndio inaonekana kazi imeisha.
Wengi wanaweza kunishushua na
kusema mbona Diamond anakinukisha kinomanoma kimataifa ? Ukweli unabaki
kuwa hata mawazo yake yanabaki kuwa Afrika ingawaje katika mahojiano
mengi husema anataka kulikuza soko la Bongo kimataifa na mipango hiyo
kweli ipo na anaonesha. Huku washindani wake nao wakiwa na mawazo mgando
mawazo yao yakibaki kugombania ma-fans
waliopo Kenya, Uganda na Afrika kwa ujumla. Unadhani kwa aina hii kweli
soko letu linakua kimataifa ?. Wakati Afrika Kusini na Nigeria
wakituongoza kimuziki kwa miaka mingi lakini miaka kadhaa tumewaua na
sisi kushika namba moja, Afrika Kusini na Nigeria sasa wamerudisha enzi
zao, kwani tayari wenzetu wanawaza mbali zaidi.
NIGERIA WAKOJE ?
Baada ya kuona Tanzania
tumekuja vizuri kimuziki, walichokifanya kutengeneza urafiki na nyota wa
Tanzania ili wazidi kupenya zaidi na waliweza kufanya hivyo, mfano
mzuri Patoranking alikuja Tanzania mwaka 2013 alipiga show ya Fiesta na Waje hivi sasa anachukua wimbo bora wa mwaka na kweli ulistahili.
KWANINI NIGERIA WANAWAZA MITA 10,000 ?
Tayari wameshatwaa ndoo za
Afrika kimuziki na wameshafanya makuu, sasa hivi tayari wamewatanguliza
wasanii wao kimataifa ili wakaliteke soko hilo akitumwa Davido, Wizkid
na Tiwa Savage huku Davido akisaini na Sony Music na tumeona kazi
alizozitoa uzuri wake ameanza na albumu, ngoma ambayo amemshirikisha
Tinashe ‘Haw long’ na sasa anatarajia kutoa ngoma nyingine katika albumu hiyo inaitwa ‘For you’ ngoma hizi tayari zimetusua huku Tiwa Savage akisainiwa na Roc Nation na tayari ametoa ngoma kali kama Buy Signal.
Unadhani kwa namna hii na
jinsi ngoma zao wanavyozipeleka hawafiki mbali ? Bado sijamtaja mnyama
mmoja anayeitwa Wizkid Ayo huyu tayari kashapenyesha ngoma zake mbele
kwani tayari zimeshakaa katika mstari mzuri. Hivyo Bongo fikirieni upya
bila hivyo mtabaki kugombania mashabiki hadi mchoke. Kumbuka
aliyeutambulisha vyema muziki wao Nigeria ni 2baba Idibia yeye ndiye
aliyebutua kopo la kombolela la Nigeria hadi leo wamefanikiwa.
SOURCE: MTEMBEZI
0 comments:
Post a Comment