Home »
» SUMATRA WAITAKA SERIKALI KUZUIA BODABODA NA BAJAJI
BARAZA
la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchikavu na Majini
(Sumatra-CCC), limeitaka serikali kusitisha usafiri wa bodaboda na
bajaji, hadi mtaala wa kuwafundisha madereva wa vyombo hivyo
utakapotungwa na kuanza kufundishwa.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk.
Oscar Kikoyo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa
mashindano ya vilabu vya wanafunzi wa Sumatra-CCC vilivyokuwa vikichuana
kuonyesha umahiri wa sheria za barabarani.
Dk.
Kikoyo alisema wakati serikali ikiruhusu bodaboda na bajaji kufanya
biashara, ilikuwa haijajiandaa kuwa na mfumo wa kutoa huduma hiyo.
“Hapakuwa na mtaala wa kuwafundisha,
kwa hiyo mtu akitaka kuendesha bodaboda anajifunzia mtaani mwenyewe siku
moja au mbili, akijiona ameweza anaingia barabarani kubeba abiria.
“Kwa hali ilivyo hivi sasa ajali ni
nyingi watu wanapoteza maisha tunaiomba serikali isimamishe kwanza
utoaji wa huduma kwa vyombo hivi ili tufanye maandalizi ya kina kuhusu
mfumo wa utoaji mafunzo kwao,” alisema.
Alieleza kuwa hiyo ni changamoto kubwa
ambayo imesababisha watanzania wengi kila siku kupoteza maisha kutokana
na ajali zinazosababishwa na kundi hilo.
“Vifo hivi sio tu vinatokea kwa abiria wanaowapandisha kwenye vyombo hivi, pia na wenyewe wamekuwa wakipoteza maisha,” alisema.
0 comments:
Post a Comment