Home »
» UKAWA WATOA TAMKO ISHU YA SUMAYE KUPEWA NOTISI YA SIKU 90
Siku
chache baada ya Serikali kumpa notisi ya siku 90 Waziri Mkuu mstaafu,
Frederick Sumaye ikimtaka kuyaendeleza mashamba yake kwa kipindi
hicho, viongozi wa Ukawa wamesema kitendo hicho ni kutengeneza chuki
endelevu na kujenga Taifa la visasi.
Juzi,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema
Sumaye amepewa siku 90 kuyaendeleza mashamba yake ya Mabwepande jijini
Dar es Salaam na Mvomero mkoani Morogoro la sivyo atafutiwa hati ya
umiliki wake.
Hata hivyo, Sumaye ambaye ni Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chadema alisema notisi hiyo ni matokeo ya chuki za
kisiasa baada ya kuihama CCM.
0 comments:
Post a Comment