Monday, 31 October 2016

KILICHOSABABISHA KIFO CHA THOMAS MASHALI PROMOTA WAKE ABAINISHA

Leo October 31 2016 zimeripotiwa taarifa za kifo cha Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali ambapo imeelezwa kuwa Marehemu Mashali alifariki usiku wa kuamkia leo maeneo ya Kimara DSM kwa kushambuliwa na watu baada ya yeye kusingiziwa ni mwizi na watu ambao aligombana nao.
Promota Siraji Kaike amesimulia tukio la Bondia Thomas Mashali kuuawa kwa kupigwa baada ya kuitwa ni mwizi, Kaike amesema 
>>>’Alitoka kwenye kikao akaenda kimara kwa rafiki yake alipofika kule jamaa wakamshawishi  akanywa bia kidogo baadaye wakahamia sijui baa gani’sasa wakagombana na jamaa, na anakuwa mtemi akilewa, jamaa wakamuitia mwizi wakampiga mapanga’
>>>’baadaye wanagundua sio mwizi tayari washampasua alama kubwa sana na tayari alikuwa ameshapungukiwa na damu nyingi sana wakawa wamemtupa baada ya hapo bodaboda walikuwa wanamjua Thomas wakamuokota na kumpeleka hospitali, mdogo wake alienda muhimbili akapewa taarifa kuwa amefariki’
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive