Home »
» SUMAYE KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE
HATIMAYE
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ameamua kukimbilia mahakamani
kutafuta haki ya shamba lake la heka 33 lililopo Mji Mpya eneo la
Mabwepande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ambalo limevamiwa na
wananchi waliogawana viwanja na kujenga makazi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Sumaye alisema mara baada ya tatizo hilo kutokea na kutumia njia za
majadiliano bila mafanikio, ameamua kufungua kesi ili kutafuta haki.Alisema kesi hiyo imefunguliwa na wakili wake na tayari hati ya kuitwa mahakamani wahusika imeshapelekwa kwao.
Mwishoni mwa mwaka jana wananchi,
wakiwamo waliobomolewa nyumba zao katika mabonde ya Mkwajuni na Msimbazi
wilayani Kinondoni, wakijikatia maeneo kwa ajili ya viwanja vya makazi
mapya.
0 comments:
Post a Comment