Home »
» MKE WA TRUMP ADAI FIDIA KWA WALIOMZUSHIA UKAHABA
Gazeti la Daily Mail la Uingereza
pamoja na blog moja ya Marekani zimeshtakiwa na mke wa Donald Trump
Melania Trump kwa kumchafua kuwa aliwahi kuwa kahaba miaka ya 1990 na
akitaka wamlipe kiasi cha $150 milioni.
Wakili wa mama huyo Charles Harder
alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitoa tuhuma kadha wa kadha kuhusu
Melania ambazo ni za uongo kwa asilimia mia moja na zenye lengo la
kumharibia mwanamke huyo ambaye mume wake atapeperusha bendera ya Chama
cha Republican katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani.
Gazeti hilo la Uingereza lilitoa
taarifa kuwa inawezekana Melania Trump aliwahi kuhudumu kama kahaba kwa
muda alipokuwa jijini New York na pia likieleza kuwa uhusiano wake na
mumewe Donald Trump ulianza mapema kuliko inavyoelezwa sasa, huku
mwanablog wa Marekani naye akieleza kuwa Melania ana hofu sana kuhusu
maisha yake ya zamani kuwekwa hadharani hususani wakati huu ambapo mume
wake anagombea urais wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi duniani.
Madai hayo ya Gazeti la Daily Maily
pamoja na blog hiyo ya Marekani yanakanushwa vibaya na Melania Trump na
kwa kupitia mwanasheria wake Charles Harder ameomba vyombo hivyo vya
habari kumlipa kiasi cha $150M na kubadilisha taarifa zao kitu ambacho
kilitekelezwa na vyombo hivyo vya habari lakini suala la kulipwa bado
halijaidhinishwa.
0 comments:
Post a Comment