Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeweka bayana majina ya
wachezaji ambao waliombewa vibali vya kushiriki katika hatua ya makundi
huku likiwepo jina la mlinzi wa zamani wa Simba Hassan Kessy ambaye kwasasa yupo Yanga.
Cloud FM kupitia kipindi chake cha michezo "Sports Extra" kilifanya
mazungumzo na afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alitoa ufafanuzi
kwanini nyota huyo hashiriki michuano hiyo wakati jina lake lipo kwenye
orodha ya majina ya wachezaji wanaotakiwa kucheza mashindano hayo ambayo
kwa sasa yanaelekea ukingoni katika hatua ya makundi
Tulipofungua usajili, Yanga walitulea majina manne likiwemo jina la
Hassan Kessy, Vicent Andrew ‘Dante’ na Beno Kakolanya na Juma Mahadhi.
Baada ya kupeleka yale majina na kwakua tulishasajili tangu tarehe 15
hadi tarehe 8 mwezi August kwamba ndiyo mwisho wa usajili tulipeleka
majina na kupokelewa kisha kazi ikafanywa mara moja na CAF kupitisha
hayo majina.
Lakini mwisho wa siku wachezaji wote akina Dante, Juma Mahadhi na
Kakolanya walikuwa na ruhusa ya kucheza kwasababu walikuwa na barua
kutoka vilabu walivyokuwa wanachezea awali (release letter).
Kessy hawezi kucheza mchezo dhidi ya MO Bejaia kwasababu Yanga bado
hawajamalizana na Simba, kwa mujibu wa barua yao iliyopo TFF, Simba
wanadai Hassan Kessy alivunja mkataba kabla ya wakati.
Kwa mujibu wa mikataba ya usajili ya kitaifa na kimataifa kuanzia
January 15 hadi June 15, Kessy alikuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo
na klabu yoyote kwasababu mkataba wake ulikuwa unaelekea kumalizika.
Lakini madai ya Simba kwa mujibu wa barua zao ni kwamba, Hassan Kessy
japokuwa alikuwa na ruhusa ya kufanya mazungumzo lakini hakuwa na ruhusa
ya kutumikia, kitendo cha kutumikia kinatafrisiriwa na Simba kwamba ni
kuvunja mkataba.
Simba wanamtuhumu Kessy kwamba alianza kushiriki shughuli za Yanga
kabla. Mazoezi na shughuli nyingine ikiwemo ile ya tarehe 25 May siku ya
Jumatano kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA ambapo Yanga ilicheza
na Azam. Kessy alikuwa upande wa Yanga na mbali na hapo alifanya mazoezi
na klabu ya Yanga kwa mujibu wa Simba ikiwa tarehe 15 ya mwezi June
bado haijafika (siku ya kumalizika kwa mkataba wake).
Baada ya fainali hiyo Simba wanaendelea kumtuhumu Kessy kuendelea na
mazoezi na klabu ya Yanga, wanasema kwamba, kati ya tarehe 12 June siku
tatu kabla ya mkataba wake kumalizika, alisafiri na Yanga kwenda Uturuki
ambapo Yanga ikwenda kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za
nane bora za kombe la shirikisho.
0 comments:
Post a Comment