Home »
» CHADEMA WAGAWA BENDERA NA JEZI KWA AJILI YA UKUTA
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimeanza kugawa
vifaa zikiwemo bendera kwa ajili maandalazi ya Umoja wa Kupinga Udikteta
( Ukuta) ambayo yanatarajia kufanyika Septemba mosi mwaka huu.
Katibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema,
Casimir Mabina, alisema kuwa bendera hizo zitaanza kupeperushwa kuanzia
kesho kutwa kwa ajili ya kuunga mkono azimio la Kamati Kuu ya kufanyika
oparesheni Ukuta.Alisema
oparesheni Ukuta ni lazima ifanyike nchi nzima na kwamba hawako tayari
kuona ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na serikali ya
awamu ya tano ambayo imeonyesha viashiria vya utawala wa kidikteta.
“Tumeona jinsi Rais alivyopiga marufuku
wapinzani kukutana kwenye mikutano ya hadhara huku akiwatishia kuwa
wakikaidi atawashughulikia na kweli amewaamuru polisi watekeleze amri
hiyo ya kuwakamata viongozi wa Chadema na kuwafungulia mashtaka,”
alisema
CREDIT-NIPASHE
0 comments:
Post a Comment