Home »
» Tume yatuma waraka mnzito kwa jeshi la polisi
TUME
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekishauri Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kusitisha maandamano yake ili kutoa
nafasi kwa mahakama kufanya kazi yake kwa umakini bila shinikizo la muda
kati ya sasa na Septemba mosi mwaka huu.
Aidha, imelishauri jeshi la Polisi
kutotumia neno ‘tutawashughulikia wote watakaokaidi amri’ kwa kuwa
imeona maneno hayo yanaweza kusababisha matumizi mabaya ya mamlaka ya
jeshi hilo.
Katika
hatua nyingine, Mahakama Kuu imetupilia mbali maombi ya wadhamini wa
Chadema ya kupinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta
Jenerali (IGP) Ernest Mangu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa
muda usiojulikana.
Mwenyekiti wa THBUB, Bahame Nyanduga
aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kumalizika kwa mkutano uliohudhuriwa na Msajili wa Vyama
vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Vincent Mashinji na washauri wake pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), Daniel Loya.
Nyanduga alisema Tume iliandaa mkutano
huo ili kuzungumzia tamko la jeshi la Polisi la Juni 7, mwaka huu la
kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa isiyo ya kiutendaji na
tamko la Chadema kuhusu Operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta
Tanzania (UKUTA) na mikutano wanayopanga kufanya Septemba mosi, mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment