Home »
» Serikali yalifungia Mseto miezi 36
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye leo Agosti
11.2016, ametangaza rasmi kulifungia gazeti la MSETO kwa miezi 36
lisichapishe Habari zake hapa nchini kwa njia yoyote ile kutokana na
kukiuka maadili ya taaluma ya Habari.
Waziri Nape Nnauye ametoa tamko hilo huku akizitaja tuhuma mbalimbali
zikiwemo: Uchochezi, Uongo na Upotoshaji ambapo hazizingatii kanuni za
taaluma ya uandishi wa habari.
Amri hiyo ya kulifungia gazeti la mseto imetokana na tangazo la
Serikali namba 242 la tarehe 10/8/2016 kwa mujibu wa sheria ya magazeti
ya mwaka 1976 sura 229 kifungu cha 25(1)
Aidha, Waziri Nape amesema gazeti hilo linaandika habari na taarifa za
uongo ambazo zina nia ya kupotosha jamii ikiwa ni pamoja na kutumia
nyaraka za serikali ambazo zimegushiwa ili kuwachafua viongozi wa
serikali na seerikali yao.
0 comments:
Post a Comment