Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kitengo cha utafiti cha
wanasayansi nchini Brazil EurekAlert, kukaa na njaa kunapelekea nywele
kurefuka kwa haraka.
Kitengo hicho katika utafiti wake, kimenukuliwa na jarida la Cell
Reports kuwa kukaa na njaa kunapelekea nywele kukuwa kwa haraka.
Utafiti huo ulifanywa kwa kutumia kundi la panya waliopewa chakula
kichache na kundi la panya waliopewa chakula kwa kiasi cha kawaida kwa
mlo wa kila siku.
Utafiti huo ulifanywa kwa muda wa miezi 6.
Katika utafiti huo panya waliopewa chakula kichache walionekana kuwa na mabadiliko katika miili huku manyoya yakiongezeka.
0 comments:
Post a Comment