LEO tutaangazia vyakula vya kuepukwa na wagonjwa wa vidonda vya tumbo
lakini pia tutaeleza vyakula vinavyofaa kuliwa na hao wenye matatizo
hayo. Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa huo wa
vidonda vya tumbo (ulcers), unapaswa kujiepusha kula vyakula vyenye
mafuta mengi na sukari nyingi.
VYAKULA VYA KUEPUKWA
Kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo anatakiwa aepuke kula vyakula aina
zote vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali
(mchanganyiko) kama sambusa za pilipili, achali (pickle), juisi ya
ukwaju, juisi ya limau n.k. Viungo vingine visivyofaa kwa mgonjwa wa
vidonda vya tumbo ni pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye
ladha ya ukali au uchachu ambavyo hutiwa ndani ya mboga au chakula ili
kuongeza ladha kama vile vinegar au tangawizi.
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine, vinaweza kuleta
matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza
pia kupatwa na tatizo hilo. Hivyo basi ni vyema wagonjwa wa vidonda vya
tumbo au hata kama huugui, inashauriwa kuepuka vyakula hivyo na kama
unavitumia basi tumia kwa kiasi kidogo kwani kwa mfano vinywaji vyenye
caffeine huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au
kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.
UHUSIANO KATI YA ULAJI CHUMVI NA VIDONDA VYA TUMBO
Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa
JINSI ULIVYO INATOKANA NA UNAVYOKULA
Vyakula vya kuepukwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo chumvi nyingi
ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye chakula
wakati wa kula, yaani chumvi mbichi inayotiwa mezani wakati wa kula si
nzuri kiafya.
Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanashauriwa kula mafuta yatokanayo na
samaki ambayo kitaalamu huitwa Omega-3 Fats ambayo yameonekana kutoa
ahueni kwa wagonjwa. Kwa mtu ambaye si mgonjwa wa vidonda vya tumbo
akila mafuta hayo atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na
magonjwa mengine ya tumbo.
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia pia
kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale
ambao hawajaathirika. Wenye vidonda vya tumbo wanashauriwa kupenda kula
matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi
mbivu na matunda mengine yenye vitamini C, hali kadhalika maziwa ya
mbuzi, jibini na cream za maziwa, kwani huleta ahueni kwa wagonjwa hao.
Sigara ni mbaya kwani huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa huo
ikiwa ni pamoja na wasiwasi. Kuepukana na maradhi hayo, watu wazingatie
ulaji sahihi ili waweze kuishi maisha ya furaha.
0 comments:
Post a Comment