Timu ya Mtibwa Sugar inaongoza ligi ikiwa na pointi 10, lakini baadhi
ya mashabiki na wadau wa soka wamekuwa wakiibeza timu hiyo kuwa
wamewashikia nafasi baadhi ya vilabu.
ShaffihDauda.co.tz imemtafuta kocha mkuu wa timu hiyo Zuber Katwila
ambaye amesema, wanaoibeza timu yake kuwa wameshika nafasi za watu
wasubiri wataona kitakachotokea.
“Mimi mwenyewe nimekuwa nikizisikia hizo taarifa watu wakitubeza
lakini wanatakiwa watambue kuwa hii ligi haina mwenyewe, kila timu
inaweza kuwa bingwa kwa hiyo kama wataendelea kutubeza bila kufanya
vizuri wataona kitakachotokea,” Katwila.
Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi
Uhuru, amesema anafanya maandalizi na kikosi chake kama mechi zingine za
ligi huku akiongeza mbinu za kumfanya atoke na ushindi.
“Ni mechi ngumu ambayo inaweza kutupandisha ama kutushusha kutokana
na pointi zetu zilivyo, lakini mimi na wenzangu tunakiandaa kikosi
vizuri kama mechi zingine, tumerudi Manungu kwa ajili ya maandalizi
zaidi na ndio maana hatujaweka kambi Dar tunataka utulivu,”.
0 comments:
Post a Comment