Wednesday 16 August 2017

NGASA AITESA YANGA



Image result for NGASA
Mjumbe wa zamani wa kamati ya mashindano ya Yanga, Athumani Kihamia amesikitishwa na kitendo cha klabu hiyo kutomsajili kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa msimu huu.
 Kihamia aliyejitoa kwenye kamati ya mashindano ya klabu hiyo kwa madai ya kubanwa na majukumu ya ukurugenzi wa jiji la Arusha, alisema kumuacha Ngassa katika kikosi chao ni sawa na kuitupa bahati iliyojileta wenyewe
 “Naheshimu uamuzi ya kamati ilikuwa na kazi kubwa ya kufanya usajili, lakini kwa maoni yangu niseme tu kumuacha mchezaji kama Ngassa aliyejileta mwenyewe si sawa kwani angeweza kuitumikia klabu kwa gharama tuitakayo sisi si kama wachezaji wengine waliokuwa wanatamka dau lao wenyewe.”
  “Kiwango alichonacho Ngassa ni sawa na Emmanuel Okwi (Simba) ambapo wangesumbuana katika nafasi hiyo, hivyo uongozi ufanye utaratibu mwingine wa kurudisha mchezaji huyo hata katika dirisha dogo kwani kusema kuwa mwalimu hamhitaji ni hoja dhaifu kwani mwalimu huwa analetewa mchezaji na kushawishiwa juu ya uwezo wake na kufanyiwa majaribio na kukubalika au kukataliwa,” alisema Kihamia.
Share:

1 comment:

  1. Uko Sahihi kabisa KIHAMIA hata mimi nisikitika sana kuhusu Mrisho Ngasa !

    ReplyDelete

Ads

Blog Archive