Uongozi
wa Yanga, umelazimika kumnunua beki Gadiel Michael kwa shilingi milioni
10 akitokea Azam FC ambapo ameshakabidhiwa nyumba ya kupanga jijini
Dar.
Beki
huyo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam
ambapo wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa aliulalamikia
uongozi wa Azam kuwatajia dau kubwa licha ya mchezaji huyo kubakisha
mkataba mfupi.
Inadaiwa
awali Yanga walitakiwa kutoa shilingi milioni 40 kabla ya kupunguziwa
na kutakiwa kutoa Sh milioni 20 ambayo bado kwao ilionekana ni nyingi
hali iliyosababisha Azam wawaambie Yanga wataje kiasi walichokua nacho,
wakamalizana kwa Sh milioni 10.
“Baada
ya majadiliano ya muda wakakubaliana kiwango hicho, Yanga wakapeleka,
wakakabidhiwa mchezaji na tayari wamempa nyumba Gadiel,” kilisema
chanzo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, kwa upande wake alisema:
“Siwezi kuzungumzia fedha ila ni kweli kwa sasa Gadiel ni mchezaji wetu
baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili na tumeshampatia nyumba
ya kuishi hapa mjini ili aweze kuifanya kazi vizuri.”
0 comments:
Post a Comment