Utulivu unashuhudiwa nchini Kenya baada ya kampeni kali wakati nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa siku ya Jumanne.
Miaka 10 iliyopita zilishuhudiwa ghasia mbaya nchini humo ambazo hakuna mtu angependa zirudie tena.
Lakini huku kura za maoni kuonyesha kuwepo kinyanganyiro kikali kati ya rais wa sasa Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinaani Raila Odinga, kuna hofu kuwa huenda kukawa na matatizo mbeleni.
Kile ambacho hufanyika nchini Kenya hakihusiani sana ni nani atakuwa mshindi bali vile wale walioshindwa watachukulia kushindwa kwao.
Mafanikio ya mifumo wa kidigitali ya tume ya uchaguzi na mipaka yatakuwa muhimu kwa uchaguzi huo kutajwa kuwa wenye huru na haki.
Ikiwa mifumo hiyo itafeli sawa na mwaka 2013 kura zitahesabiwa kwa mikono, na katika nchi ambayo imekubwa na madai ya wizi wa kura bado yule ambaye atashindwa atapinga matokeo hayo.
Mwaka 2013 Raila Odinga alidaia kuwepo udanganyifu na alipoteza kesi mahakamani.
Wakati huu, akiwa anawania kwa muhula wa nne na hasa mara ya mwisho, anaweza akaingia mitaani ikiwa atahisi kuwa kura hizo zimeibiwa.
Kuuliwa kwa meneja wa masuala ya kompiuta wiki moja kabla ya uchaguzi ni kisa kimezua wasi wasi nchi Kenya
Chris Msando alikuwa akisimamia mifumo ya eletroniki na alionekana kwenye runinga akihakikishia umma kuwa mifumo hiyo itafanikiwa na haiwezi kudukuliwa.
Wakati mwili wakae uliokuwa na majera mabaya ulipatikana kwenye kichaka, madai yaliibuka kuwa kuna mtu alikuwa anapanga kuingilia kati uchaguzi.
Ikiwa hakuna mgombea atashinda kwa zaidi ya asilimia 50, basi uchaguzi utaelekea duru ya pili. Lakini kutokana na kutowepo mgombea maarufu wa tatu hizi inaonekana kuwa mbio za farasi wawiili.
Chochote kile kitakachotokea, hizi zitakuwa mbio za mwisho za Uhuru Kenyatta mtoto wa rais wa kwanz wa Kenya dhidi na Raila Odinga ,mtoto wa makamu wa kwanza wa raia wa Kenya.
Kenyatta mwenye umri wa miaka 55 anataka kuingoza kwa muhula wa pilia na wa mwisho kupitia chama cha Jubilee baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2013, licha ya kukabiliwa na kesi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Bwana Kenyatta ambaye anatoka jamii ya Kikuyu na hasimu wake wa zamani William Ruto kutoka jami ya Kalenjin, walilaumiwa kwa kuchochea ghasia kati ya jamii hizo.
Mashtaka yao yalihusiana na ghasia za baada ya Uchaguzi wa 2007 ambapo karibu watu 1200 waliuawa na kuwalazimu wengine maelfu kuhama makwao.
0 comments:
Post a Comment