Tuesday, 29 August 2017

SOUARE AREJEA TENA BAADA YA KUKAA NJE KWA MUDA MREFU

Pape SouareHaki miliki ya pich
Beki wa Crystal Palace Pape Souare amerejea uwanjan toka alipopata ajali mbaya ya gari na kusababisha kuvunjika mfupa wa nyonga na taya.
Souare mwenye umri wa miaka 27 alipata ajali ya gari mwezi Septemba mwaka 2016 na alirejea mazoezi na klabu yake mwanzoni mwa mwezi huu.
Mlinzi huyo wa kulia raia wa Senegal alicheza kwa dakika arobaini na tano akiwa na kikosi cha chini ya umri wa miaka 23 cha timu yake dhidi ya Nottingham Forest.
Crystal Palace walipoteza mchezo huo kwa kufungwa kwa mabao 2-1 na baada ya mchezo Souare aliandika katika ukurasa wake wa mtandao Twita " Nina furaha kupata dakika kadhaa kucheza nahisi vizuri."
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive