Monday, 7 August 2017

MALAYSIA,POLISI WAKUPAMBANA NA UGAIDI WAWAKAMATA WATU 400


Security drill for the upcoming South East Asian Games in Kuala Lumpur, Malaysia, 20 July 2017Haki miliki ya picha

Zaidi ya watu 400 wamekamatwa katika oparesheni dhidi ya ugaidi nchini Malaysia.
Wale waliokamatwa katika mji mkuu Kuala Lumpur walikuwa ni kutoka nchini Bangladesh, India na Pakistan.
Vifaa vya kutumika kutengeneza passport bandia na kupata stakabadhi zisizo halali za uhamiaji za Malaysia, ni kati ya vifaa vilivyonaswa.
Usalama unaimariswa mjini humo kabla ya mashindania ya nchi na kusini mashariki mwa Asia yanayotarajiwa kuanza muda wa wiki moja inayokuja.
Mamlaka zinasema kuwa zinalenga yeyote asiye na stakadhi za usafiri na yeyote ambaye anaaminika kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq.
"Tutawatambua na kuwachukulia hatua wageni wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na magaidi, hasa wanaohusika na mambo tofauti nchini Syria," afisa wa kupambana na ugaidi Ayob Khan Pitchay alisema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive