Tuesday 1 August 2017

MAJALIWA AAGIZA MEYA WA JIJI LA MBEYA AKAMATWE


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwakamate watendaji 12 wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiwamo aliyekuwa mstahiki meya Athanas Kapuga.


Amesema pia wakamatwe, wakurugenzi watatu, kaimu mkurugenzi, wahasibu wawili na wajumbe wa bodi wanne kwa kuisababishia hasara jiji hilo kiasi cha Sh63 bilioni katika ujenzi wa Soko la Mwanjelwa.

Amewataka makamanda wa Takukuru kuanzia leo wawakamate watuhumiwa hao na kwamba anatuma timu kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuandaa mashtaka hayo ambapo itatua Mbeya kesho Jumatano.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive