Riyad Mahrez ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya kikosi cha Algeria na kurudi Ulaya ili kukamilisha uhamisho wake hadi klabu mpya kulingana na shirikisho la soka nchini Algeria.
Winga huyo wa Leicester aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika uwanja wa King Power na amehusishwa na vilabu vingi huku Roma ikiwa tayari imewasilisha ombi la kumununua mchezaji huyo mara tatu , ombi la mwisho likiwa lile la dau la £32m.
Klabu kama vile Barcelona, Arsenal, Manchester United na Chelsea zimeripotiwa kutaka kumsajili Mahrez ambaye alikuwa mchezaji bora 2016 baada ya kuwa kiungo muhimu wa timu ya Leicester ilioshinda kombe la ligi ya Uingereza msimu huo.
0 comments:
Post a Comment