Saturday, 26 August 2017

MAGUFULI AANZISHA TIMBWILI CCM


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, amewapiga pini vigogo wa chama chake walijilimbikizia mali kwa kuhujumu rasilimali za chama hicho kwa kuwaambia kuwa siku zao zinahesabika.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alisema ana taarifa zote kuhusiana na wale waliotanguliza maslahi binafsi kwa kujilimbikizia mali za CCM na kwamba anasubiri muda ufike ili awashughulikie.

Rais Magufuli aliyasema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo la kivuko cha Feri na kisha kuvuka bahari kwa kutumia kivuko cha MV Kigamboni, ambako alikutana na wananchi wa eneo hilo na kisha kutembelea Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Katika chuo hicho, Rais Magufuli alikutana na vijana wa CCM kutoka vyuo vya mkoa wa Dar es Salaam waliopiga kambi katika chuo hicho.

Rais Magufuli aliwaambia viongozi wa sekretarieti ya CCM aliowakuta wakizungumza na vijana hao wa chama tawala kuwa tayari anazo taarifa za watu waliojimilikisha mali za chama, hivyo wajue wakati wa kuwashughulikia unakuja.

Tangu atwae uenyekiti wa CCM Julai 23, mwaka jana, Rais Magufuli amekuwa akisitiza dhamira yake ya kupambana na rushwa ndani ya CCM nyakati za uchaguzi na pia kukomesha vitendo vya kuhujumu mali za chama vinavyofanywa na baadhi ya makada wake wasio waaminifu.

Akiwa chuoni, Rais Magufuli alikutana na vijana wa CCM kutoka vyuo na vyuo vikuu vya mkoa wa Dar es Salaam waliopiga kambi katika chuo hicho, ambao walimpongeza kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuiongoza serikali ya awamu ya tano
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive