Tuesday 22 August 2017

LISSU AGOMA KUTOA MAELEZO POLISI


Image result for tundu lissu


Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amehojiwa kwa tuhuma za kufanya makosa 2 kosa la kumkashifu Rais kwa kusema makosa yake hadharani na kosa la uchochezi kuhusu kuzuiliwa ndege ya serikali, hata hivyo Tundu Lissu amegoma kutoa maelezo polisi.




Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekataa kutoa maelezo yoyote polisi, akitumia haki yake ya kisheria kuwa mtuhumiwa ana haki kisheria, kutaja jina na anuani yake tu anapokuwa anashikiliwa na polisi hadi atakapopelekwa mahakamani ambako ndiko atataoa maelezo kujibu mashtaka anayotuhumiwa nayo.

Tundu Lissu akiwa polisi hapo alipata msaada wa kisheria kutoka kwa Wakili Faraji Mangula, ambaye pia anashughulikia uwezekano wa mteja wake kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo Chama Cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA kimesema kimeshatoa maelekezo kwa wanasheria wa chama hicho kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria iwapo Jeshi la Polisi halitampeleka mbele ya mahakama Tundu Lissu ndani ya muda unaoagizwa na sheria za nchi. 

Mbali na hilo CHADEMA kimeendelea kusisitiza kuwa serikali bado inawajibu wa kujibu hoja za msingi zilizotolewa na chama hicho kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu kama ambavyo walisema kwenye mkutano na vyombo vya habari.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive