Wednesday, 9 August 2017

HAJAKUBWA YAMCHONGEA MWIZI KUTAMBULIKA MAREKANI

Andrew Jensen alikamatwa mnamo mwezi Julai 28 mwaka mmoja baada ya uvamizi mwengine wa nyumba moja mnamo mwezi Oktoba 2016.Haki miliki ya picha
Mwizi mmoja amekamatwa baada ya maafisa wa polisi kusema kuwa aliwacha ushahidi muhimu katika eneo la wizi baada ya kushindwa kusafisha choo alichotumia kwenda haja.
Wachunguzi wanasema kuwa sampuli za mikojo za Andrew Jensen katika nyumba hiyo ya Los Angeles ya Thousand Oak inafanana na vinasaba vya data ya FBI.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 42 alikamatwa mnamo mwezi Julai 28 mwaka mmoja baada ya uvamizi mwengine wa nyumba moja mnamo mwezi Oktoba 2016.
Polisi wanasema kuwa wanakusanya ushahidi uliowachwa katika eneo la uhalifu.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Ventura Tim Lohman alisema kuwa alifanya haja na hakusaficha choo.
''Watu wengine hawajui kwamba DNA zinaweza kupatikana kupitia maeneo mengine mbali na mate na nywele''.
''Tunachunguza ushahidi wowote ambao umewachwa.Iwe sigara iliovutwa, ama mkebe ambao umewachwa nyuma ,tutautathimini''.
Bwana Jensen ambaye aliwachiliwa huru kwa dola 70,000 anazuiliwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive