STRAIKA mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku ameanza kazi klabuni hapo baada ya kukamilisha mchakato wa usajili akitokea Everton na
kuamua kuchagua jezi namba 9. Lukaku amesema amechagua jezi hiyo kwa
kuwa yeye ni straika halisi na nyuma ya pazia ni kuwa aliomba ruhusa ya
kuivaa jezi hiyo kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye ndiye aliyekuwa akiivaa msimu uliopita.
Iliaminika kuwa Lukaku ataichagua jezi namba 10 ambayo iliachwa na
aliyekuwa nahodha, Wayne Rooney lakini ameipotezea. “Nimekuwa na kawaida
ya kumuuliza mama yangu ni namba ipi ya kuvaa, nilizoea kuvaa namba 10
kwa kuwa siku ya kuzaliwa ya mama
aliyezaliwa Oktoba 10. “Nimeamua kubadili namba na sasa nitavaa namba
9 kwa kuwa mimi ni straika, ni namba nzuri na niliomba ruhusha hiyo kwa
Zlatan Ibrahimovic. “Namshukuru kwa kuniruhusu kuivaa,” alisema Lukaku
licha ya kuwa kwa sasa Zlatan hayupo kwenye kikosi hicho.
Ibrahimovic aliichukua namba 9 kutoka kwa Anthony Martial alipojiunga
United msimu uliopita na amefunga mabao 28 kabla ya kuumia goti Aprili,
mwaka huu. Lukaku ametua United kwa pauni milioni 75 (Sh bilioni
213.9), atakuwa akilipwa pauni 200,000 (Sh milioni 570.6) kwa wiki,
ameungana na wenzake moja kwa moja Los Angeles, Marekani ambapo ndipo
timu ilipoweka kambi kujiandaa na msimu mpya
0 comments:
Post a Comment