Wednesday, 5 July 2017

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO 05.07.2017

Alexandre Lacazette


Haki miliki ya picha

Alexandre Lacazette amekamilisha vipimo vya afya Emirates na mkataba wake wa miaka mitano wa pauni milioni 52 unatazamiwa kuthibitishwa baadaye leo (BBC, Sky).
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, 31, ameondolewa kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda Marekani, na atakamilisha uhamisho wake wa bila malipo kurejea Everton mwishoni mwa wiki. Everton pia wanataka kumsajili Olivier Giroud, 20, kutoka Arsenal kwa pauni milioni 20 (Sun).
    Manchester United wanataka kupanda dau jipya kumtaka winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28 (Sky Italia).
    Manchester United watafanya jaribio la mwisho kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, wiki hii, huku Real wakigoma kushusha bei ya pauni milioni 72 (Independent).
    Beki wa Roma Antonio Rudiger, 24, amewasili London kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Chelsea (Daily Mirror).
    Chelsea wanafikiria kumchukua pia kipa wa Paris Saint-Germain Alphonse Areola, 24 (Transfermarketweb).
    Manchester City wamekataa ombi la Newcastle United kumchukua kipa Joe Hart, 30, kwa mkopo (Daily Mail).

    Joe HartHaki miliki ya picha

    Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, ametoa sharti la kuwa mchezaji anayelipwa zaidi- nyuma tu ya Cristiano Ronaldo- iwapo Real Madrid wanataka kumsajili (Diario Gol).
    Meneja wa Leicester City ametoa dau la pauni milioni 20 kumtaka mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 29 (Daily Mirror).
    Tottenham wanataka kumchukua kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, lakini hawapo tayari kulipa pauni milioni 50 wanazotaka Everton (Sun).
      Liverpool wametoa dau la pauni milioni 14.9 kutaka kumsajili beki wa Lyon Emanuel Mammana, 21 (Sport Review).
      Juventus wamempa beki wao Alex Sandro, 26, mshahara wa pauni 84,000 kwa wiki ili kumshawishi asiondoke kwenda Chelsea ambao wapo tayari kutoa pauni milioni 61 kumnunua (London Evening Standard).
      Kiungo wa Arsenal Santi Carzola, 32, ambaye hajacheza tangu Oktoba 2016, huenda akakosa msimu ujao wote wa 2017/18 kutokana na kuwa majeruhi bado (Daily Express).
      Beki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka, lakini meneja Arsene Wenger amekataa ombi lake la kutaka kuondoka. Barcelona wanataka kumsajili beki huyo kwa pauni milioni 35 (Daily Express).
      Tottenham wanataka kumsajili Alfie Mawson, 23, kutoka Swansea, au Ben Gibson, 24, kutoka Middlesbrough, huku wakitaka kumuuza beki wao wa kati Kevin Wimmer, 24 kwa pauni milioni 20 (Daily Mirror).
      Dau la pauni milioni 8 kumsajili mshambuliaji Britt Assombalonga, 24, limekataliwa na Nottingham Forest (Daily Mail).

      Santi CazorlaHaki miliki ya picha

      Crystal Palace wanafikiria kusajili mabeki wawili Joel Veltman, 25, na Kenny Tete, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 10 (Guardian).
      Newcastle wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26 (Shields Gazette).
      Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Uingereza
      Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.
      Share:

      0 comments:

      Post a Comment

      Ads

      Blog Archive