Thursday, 6 July 2017

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 6/7/2017 NA DENIS MASSAWE

Manchester United wamewapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24, kwa kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 75 (Daily Mail).
Manchester United wametoa dau la pauni milioni 66 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, na huenda makubaliano kati ya timu hizo mbili yakafikiwa katika saa chache zijazo (Marca).
Manchester United wangependa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Julian Weigl baada ya kushindwa kuwapata Eric Dier kutoka Tottenham na Nemanja Matic kutoka Chelsea (Daily Mail).

Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 (Le10 Sport).
Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau rasmi la pauni milioni 22 kutaka kumsajili Diego Costa, 28, kutoka Chelsea (Guardian).


Hatua ya Atletico Madrid kutaka kumsajili tena Diego Costa itategemea kama wataruhusiwa kumpeleka China kwa mkopo hadi adhabu yao ya usajili itakapomalizika mwezi Januari (Mirror).
Chelsea wamefikia makubaliano na Roma ya kumsajili beki Antonio Rudiger, 24 kwa pauni milioni 34, ingawa mchezaji huyo bado hajafikia makubaliano rasmi kuhusu maslahi binafsi (Sky Sports).
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier anasema Arsenal huenda wamempata 'Ian Wright mpya' baada ya kumsajili Alexandre Lacazette (TalkSport).
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, ambao ni ongezeko la pauni 125,000 kwa wiki katika mshahara wake wa sasa (Daily Mirror).

Arsenal wametoa dau jipya kwa Monaco kutaka kumsajili winga Thomas Lemar (Evening Standard).
West Ham wanaonekana kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, kwa pauni milioni 15 (Evening Standard).
Huddersfiled waliopanda daraja EPL wanakaribia kumsajili beki Mathias Jorgensen, 27, kutoka FC Copenhagen kwa pauni milioni 3.5 (Sun).
Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anazungumza na Watford kutaka kuhamia katika timu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu wa 2012-13 (Daily Mirror).



Dau la pauni milioni 3 la Burnley la kumtaka mshambuliaji wa Stoke City Jonathan Walters limekubaliwa (Sky Sports).

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive