MSHAMBULIAJI wa Yanga,Amissi Tambwe ametamka kuwa Mrundi mwenzake Yusuph Ndikumana anakuja Jangwani.
Kauli hiyo, ameitoa baada ya kuwepo
tetesi kuwa wakala wake amekwamisha usajili wa kiungo huyo kutokana na
kutofikia muafaka mzuri na Yanga huku ikielezwa anarejea Mbao FC.
Ndikumana ni kati ya wachezaji
waliokuwepo kwenye orodha ya usajili wa wachezaji wanaotajwa kwenye
usajili wa timu hiyo watakaochukua nafasi ya Mzambia, Justine Zulu.
Akizungumza na Championi Jumatatu,Tambwe
alisema akiwa nyumbani kwao katika mapumziko alikutana na Ndikumana na
kumuahidi anakuja kuichezea Yanga baada ya kufikia makubaliano na
mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Tambwe alisema ujio wa kiungo huyo
utaimarisha safu ya kiungo namba 6 kutokana na uwezo wake mkubwa wa
kukaba na kuchezesha timu.
“Ndikumana haendi popote na badala yake anakuja kuichezea Yanga msimu ujao wa ligi kuu. Yeye mwenyewe aliniambia tulipokutana nyumbani Burundi wakati wa likizo na kuzungumza mambo mengi.
“Kikubwa aliniahidi kutua kuichezea Yanga
baada ya kufikia muafaka mzuri kati ya wakala wake na viongozi wa
Yanga, ninaamini ujio wake utaiimarisha timu yetu,” alisema Tambwe.
0 comments:
Post a Comment