Saudi Arabia na nchi tatu za kiarabu zimeongeza muda kwa nchi ya Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.
Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika siku ya Jumapili.
Taifa hilo la ghuba linasema kuwa litajibu kupitia barua ambayo itawasilishwa kwa Kuwait leo Jumatatu.
Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini humo, atasafiri kuenda Kuwait leo, kuwasilisha barua hiyo iliyotumwa kutoka kwa emir wa Qatar kuenda kwa emir wa kuwait ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa mzozo huo.
Siku ya Jumamosi waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, alisema kuwa taifa hilo lilikataa masharti hayo lakini liko tayari kwa mazungumzo.
Qatar imekuwa chini na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa wiki kadha sasa, kuetoka Saudi Arabia, Misri, milki ya nchi za kiarabu na Bahrain.
0 comments:
Post a Comment