Siku moja baada ya club ya Arsenal kutangaza kumsajili
mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea Olympique
Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette, leo July 6 mshambuliaji wa Arsenal
raia wa Chile Alex Sanchez ameripotiwa kutaja mapendekezo yake ili
asaini mkataba mpya.
Sanchez ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea FC Barcelona
ya Hispania, ametajwa kudai alipwe mshahara wa pound 400000 kwa wiki
ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.1 ili asaini mkataba mpya wa kuendelea
kuitumikia Arsenal.
Inaripotiwa kuwa Arsenal wapo tayari kumlipa Sanchez zaidi ya pound
275000 ambazo inaripotiwa ameahidiwa na Man City wakati FC Bayern Munich
ambao wanamuhitaji wanasitasita kutoa ofa ya kiasi hicho cha mshahara
licha ya kuonesha dhamira ya wazi ya kuhitaji huduma yake.
0 comments:
Post a Comment