BAADA ya kukaa kimya kwa miaka miwili, hatimaye lile shindano kubwa
la urembo lijulikanalo kama Miss Grand Tanzania limerudi tena kwa
kishindo ambapo safari hii linatarajiwa kufanyika Agosti 11, mwaka huu.
Akizungumza na Showbiz, mmoja wa waratibu
wa shindano hilo, Abrahamu Mahimbo alisema kuwa, kila kitu kinaenda sawa
na kwa mara ya kwanza katika historia ya shindano hilo kubwa duniani,
wanatarajia kuwa na ugeni mkubwa ukiongozwa na Mshindi wa Miss Grand
International 2016, Ariska Putri Pertiwi kutoka Indonesia akiwa na kruu
yake.
“Hadi sasa tumepata washiriki 28 ambao tutakuwa nao hadi siku ya
fainali Agosti 11 na mshindi atapata tikiketi ya moja kwa moja kuingia
katika fainali zitakazofanyika Vietnam kwenye Ukumbi wa Vinpearl Phu
Quoc Resort & Villas Convention.
Ariska Putri Pertiwi akishika ngao ya ushindi.
Tunatarajia shindano la safari hii kuwa na mvuto zaidi kutokana na uwepo wa washiriki wenye sifa tunazozitaka so safari hii huenda mshindi wa Tanzania akaibuka na kuwa Miss Grand International huko Vietnam,” alisema Abrahamu.
0 comments:
Post a Comment