Sunday 30 July 2017

MEXME AMESEMA ANAWATAKA SIMBA NA YANGA UWANJANI YEYE MANENO HATAKI


Image result for mexme kagera

 Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema hatishwi na usajili uliofanywa Simba na Yanga, alichoziambia klabu hizo ni kwamba wakutane uwanjani ambako ni kipimo cha mbwembwe zao.
"Kilichotawala katika vijiwe vya watu wa soka ni mastaa wa Simba na Yanga, ila nawakumbusha kwamba kazi ni uwanjani, isije ikafika hatua wakaanza kuhaha kana kwamba si wale ambao wanatembea kifua mbele kwa sasa," alisema.

Maxime alisema huduma bora ya mchezaji inatokana na kujua majukumu yake uwanjani, jambo analodai kwamba ndilo analifanyia kazi mazoezini kuhakikisha kila mmoja anasimama kwenye majukumu yake na anayafanya kwa asilimia mia.

"Chunguza kwa umakini asilimia kubwa ya wachezaji wazawa,wanaotamba Simba na Yanga ni wale ambao wametoka Kagera, Mtibwa, Mbeya City na timu mbalimbali za mikoani, hii ni kwa sababu hazina kasumba ya kuwekeza katika kusaka wachezaji,"anasema.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive