Wednesday 26 July 2017

MAREKANI YAWAZUIA MAAFISA VENEZUELA

US Treasury Secretary Steve Mnuchin in Washington, DC, on 26 July 2017Haki miliki ya picha

Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maafisa 13 wa vyeo vya juu nchini Venezuela wakati shinikizo zinazidi kuongezeka dhidi ya Rais Nicolas Maduro kabla ya kura inayokumbwa na utata ya bunge jipya la kubuni katika mpya.
Vikwazo hivyo ni vya kutwaliwa mali ya maafisa hao nchini Marekani na kuyazuia makampuni ya Marekani kufanya biashara nao.
Wale waliolengwa ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa majeshi.
Wiki iliyopita, Rais Donald Trump aliapa kuchukua hatua kali za kiuchumi ikiwa Bwana Maduri ataandaa kura hiyo ya maoni siku ya Jumapili.

President of Venezuela, Nicolas Maduro, speaking to supporters in Caracas, Venezuela, on 25 July 2017.Haki miliki ya picha

Hata bwana Maduro ametaja vikwazo hivyo kuwa vilivyo kinyume na sheria
Vikwazo hivyo pia vinamlenga mkuu wa baraza la uchaguzi Tibisay Lucena, aliyekuwa makamu wa rais Elias Jaua ambaye anaongoza tume zinaoandaa uchaguzi wa Jumapili.
Kujumuishwa kwa maafisa wa vyeo vya juu kutoka kwa kampuni ya serikali ya mafuta PDVSA na ishara kuwa huenda vikwazo hivyo pia vikalenga sekta ya mafuta nchini Venezuela.
Akitangaza vikwazo hivyo waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin alisema kuwa Marekani hauweza kupuuza jitihada za utawala wa Maduro za kuhujumu demokrasia, uhuru na sheria.

A demonstrator prepares to throw a tear gas canister during a strike called to protest against Venezuelan President Nicolas Maduro's government in Caracas, Venezuela on 26 July, 2017.Haki miliki ya picha
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive