Saturday, 1 July 2017

MAREKANI, WALIOBADILISHA JINSIA KUAJIRIWA JESHINI

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis


Haki miliki ya picha

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amechelewesha kuidhinishwa kwa mpango wa rais Obama wa watu waliobadili jinsia kujiunga na jeshi la Marekani.
Sera hiyo mpya itakayowaruhusu wanajeshi kubadili jinsia huku wakiendelea kuhudumu na kuweka viwango vya matibabu sasa itaanza kutekelezwa mnamo mwezi Januari 1 2018.
Maafisa wa Pentagon wanasema kuwa huduma tofauti hazijakubaliana kuhusu ni lini kuwakubali walioajiriwa.
Wanaharakati wanasema kuwa hawafurahishwi na kucheleweshwa huko

Mwanamume aliyebadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke
Image captionMwanamume aliyebadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke

''Kila siku inayopita bila sera hiyo inazuia uwezo wa jeshi wa kuwasajili wanajeshi wazuri na werevu bila kujali jinsia'', ,alisema msemaji wa shirika la haki za kibinaadamu Stephen Peters.
Katika taarifa Bwana Mattis alisema katika barua ilionukuliwa na gazeti la Washington post kwamba ameamua muda zaidi unahitajika kufanya uamuzi baada ya kushauriana na maafisa wa ulinzi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive