Haji Manara.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara.
Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya Manara
kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa
kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh
milioni 9.
Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari
leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na
kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa
kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi.
Mbali na Manara, kamati hiyo pia
imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy
Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Rukwa, James Makwinya na
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Rukwa, Ayubu Nyaulingo, ambao walikuwa
wamefungiwa kutokana na kufanya uchaguzi wakati TFF iliwazuia.
Katika hatua nyingine, Tarimba amesema
kuhusiana na adhabu ya Damas Ndumbaro, imeshindwa kupitiwa kutokana na
kutopokea ombi la kuipitia, huku pia akiiomba TFF kuangalia kama kuna
barua za watu mbalimbali walioomba kupitiwa kwa adhabu zao wazifikishe
kwenye kamati yake ili waweze kuzifanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment