Friday 21 July 2017

MAN U YAICHAPA MAN CITY LUKAKU & RASHFORD HATARI


Brahim Diaz (kushoto) akichuana na Lingard wa Manchester United.
 
Manchester United imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester City katika derby ya kwanza ugenini huku ziara za 2017 zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi The Red Devils.
 
Kyle Walker (kushoto) akichuana na Rashford.
 
Romelu Lukaku na Marcus Rashford waliisaidia United katika mabao yote mawili yaliofungwa katika kipindi cha kwanza.

Lukaku akishangilia bao lake.
 
Kikosi hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya eneo la hatari ,United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson.

pogba na Lukaku wakishangilia.
 
David De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling.

Lukaku baada ya kutupia bao.
 
United hatahivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na kucheka na wavu.

Lukaku na Rashford wakishangilia.
 
Dakika mbili baadaye Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan.
 
Kocha Guardiola wa Man City akihimiza vijana wake.
 
MAN UTD (4-2-3-1): De Gea (Romero 46); Valencia (Fosu-Mensah 78), Lindelof (Bailly 46), Smalling (Jones 46), Blind (Darmian 46); Herrera (Carrick 62), Pogba; Lingard (A Pereira 78), Mkhitaryan (Fellaini 62), Rashford (Martial 62); Lukaku. Subs: J Pereira, Mitchell, Tuanzebe, McTominay.
Scorers: Lukaku 37, Rashford 39
Booked: Blind.
 
 
MAN CITY: Ederson; Walker, Kompany (Stones 46), Adarabioyo (Otemandi), Fernandinho (Mangala 46); Toure; Roberts (Diaz 46), De Bruyne (Nasri 46), Foden (Zinchenko 74), Sterling (Sane 46); Aguero (Gabriel Jesus 46). Subs: Denayer, Kolarov, Fernando.
Booked: Toure, Mangala
Referee: Ismail Elfath
Attendance: 67,401
 
Star man: Romelu Lukaku
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive