Wednesday, 26 July 2017

LUKAKU AAHIDI KUWEKA HISTORIA OT

Mshambuliaji mpya wa Manchester United Romelu LukakuHaki miliki ya picha
Romelu Lukaku anasema kuwa anataka kuweka historia ya kipekee katika klabu ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 alijunga na Red Devils kwa kitita cha pauni milioni 75 mapema mwezi huu baada ya kuifungia Everton mabao 25 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita.
Lukaku ambaye ndio mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga mabao 80 katika ligi ya Uingereza kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 24 alisema: Siwezi kusema kwamba mimi ndio mchezaji kamili.
''Nina kazi nyingi ya kufanya na nafurahi inamaanisha kwamba ninaweza kuwa bora zaidi ya sasa''.
Hatua ya Lukaku ya kujiunga na manchesyter united inamaanisha kwamba anajiunga na kocha Mourinho ambaye alikuwa meneja wa Chelsea wakati alipomuuza Everton kwa pauni ,milioni 28 mnamo mwezi Juali 2014.
Wiki iliopita ,Mourinho aliombwa kumlinganisha Lukaku na Didier Drogba aliyefunga mabao 157 katika mechi 341 wakati wake akiichezea Chelsea , na kuweza kushinda mataji matatu ya ligi na kombe la vilabu bingwa.
Kocha huyo alisema: Siwezi kulinganisha kabisa kwa sababu mmoja ana historia yake na mwengine anaanza historia yake.
Lukaku alisema kwamba yeye na Drogba ni wachezaji tofauti .
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive