Tuesday, 4 July 2017

KOREA KASKAZINI: KOMBORA LETU LINAWEZA KUFIKA MAREKANI

Korea Kaskazini ilitoa picha za kombira hilo la masafa marefu ICBM likirushwa

Haki miliki ya picha

Marekani imethibitisha kwamba Korea kaskazini ilifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo kulingana na wataalama wanaamini linaweza kufika Alaska Marekani.
Waziri wa maswala ya kigeni amelitaja jaribio hilo kuwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia na kuonya kwamba Washington haitakubali hatua ya Korea Kaskazini kujihami na nyuklia.
Pyongyang imedai siku ya Jumanne kwamba ilifanikiwa kulifanyia majaribi kombora lake la masafa marefu ICBM.
Wakijibu, Marekani na Korea Kusini zilirusha makombora kusini mwa maji Korea.
Zoezi hilo la kijeshi la pamoja lililenga kuonyesha uwezo wa mashambulizi ya mataifa hayo mawili, Pentago imesema.
    Ijapokuwa jaribio la Jumanne lilionekana kuwa hatua kubwa ,wataalam wanaamini kwamba Korea kaskazini haina kombora la masafa marefu la kinyuklia.
    Bwana Tillerson pia alionya kwamba taifa lolote ambalo linasaidia kiuchumi na kijeshi Korea kaskazini ama limefeli kuidhinisha kwa ukamilifu maamuzi ya baraza la usalama ya Umoja wa Mataifa linasaidia utawala hatari.
    Marekani imetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kujadili swala hilo.
    Mkutano wa faragha wa wanachama wa baraza hilo unatarajiwa baadaye siku ya Jumatano.
    Je Korea kaskazini ilisema nini siku ya Jumanne?
    Tangazo hilo katika runinga ya taifa ya Korea kaskazini lilisema kuwa kombora hilo aina ya Hwasong -14 linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine lilisimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
    Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-unHaki miliki ya picha
    Ilisema kuwa kombora hilo liliruka umbali wa kilomita 2,802 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.
    Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani.
      Chombo cha habari cha Korea kaskazini KCNA baadaye kilimnukuu Kim jong un akisema kuwa jaribio hilo ni zawadi kwa Wamerakani siku yao ya uhuru.
      Jaribio hilo ambalo ni miongoni mwa majaribio ya makombora yake linakiuka marufuku ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
      Lakini wataalam wengi wanaamini kwamba Pyongyang bado haijakuwa na uwezo wa kutengeza kichwa cha kinyuklia kinachoweza kutosha katika kombora la masafa marefu na kwamba kombora kama hilo haliwezi kushambulia eneo linalolenga.
      Je kombora hilo lina uwezo wa kusafiri umbali gani?
      Swala kuu ni linaweza kusafiri kwa umbali gani, alisema mwandishi wa BBC Evans Seoul.
      Je linaweza kushambulia Marekani?.
      David Wright , kutoka muungano wa kisayansi anasema kuwa iwapo ripoti hiyo ni ya sawa ,kombora hilo linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 6.700.
      ''Umbali huo unaweza kulifanya kufika Alaska, lakini sio visiwa vya Hawaii ama hata majimbo mengine 48 ya Marekani'',alisema.
      ''Sio kombora pekee ambalo Korea Kaskazini itahitaji'', mwandishi huyo anasema.
      Pia ni lazime iwe na uwezo wa kulinda kichwa cha nyuklia kinapopaa angani na sio wazi iwapo Korea kaskazini ina uwezo huo.
      Share:

      0 comments:

      Post a Comment

      Ads

      Blog Archive