Aliyekuwa Ofisa wa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro.
KATIBU Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, jana amemtambulisha rasmi, Dismas Ten kuwa Ofisa wa Habari wa klabu hiyo. Kabla ya utambulisho huo, Dismas alikuwa ofisa habari wa Mbeya City ya Mbeya ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Bara kama Yanga.
Ofisa wa Habari wa klabu Yanga, Dismas Ten.
Hii ina maana kuwa, Yanga haitakuwa tena na aliyekuwa ofisa wa habari wake, Jerry Muro
ambaye hivi karibuni alimaliza kifungo chake cha kufungiwa mwaka mmoja
alichopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Jerry alifungiwa na
Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya mwenyekiti
wake, Wakili Wilson Ogunde kwa kosa la kudharau uamuzi wa Kamati ya
Nidhamu ya shirikisho hilo. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Mkwasa alisema amemtambulisha Dismas baada ya ofisa huyo kumaliza
mkataba wake wa miaka minne Mbeya City. “Nichukue nafasi hii kumtangaza
Dismas kuwa ndiye ofisa wetu wa habari mpya atakayefanya kazi pamoja
na Chicharito (Godlisten). “Hiyo yote ni katika kukiboresha kitengo
chetu cha habari cha Yanga ili kifanye kazi yake vizuri ndani ya klabu
yetu,” alisema Mkwasa.
Duu!mbona kazi sasa.
ReplyDelete