Tuesday, 25 July 2017

JARIBIO LA KIFAA KINACHOWALINDA WANAWAKE NA HIV LAFANIKIWA

Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.Haki miliki ya picha
Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.
Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.
Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi , ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.
Wanawake na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive