Kukamatwa kwa mbunge wa upinzani
nchini Tanzania Halima Mdee kwa madai ya kumtusi rais John Magufuli
kumeshutumiwa pakubwa huku wakosoaji wakisema kuwa ni ishara ya hivi
karibuni kwamba serikali inatumia mamlaka yake vibaya ili kukandamiza
uhuru wa kujieleza.
Msemaji wa chama cha upinzani Chadema Tumaini
Makene ameambia BBC kwamba chama hicho kitakwenda mahakamani dhidi ya
hatua ya mkuu wa Wilaya ambae aliagiza kukamatwa kwake pamoja na
makamishna wengine wote wanaokiuka sheria.
Bi Mdee ni mwanachama wa Chadema, chama kikuu cha upinzani katika aifa hilo la Afrika mashariki.
Alituhumiwa
na Ally Hapi, mkuu wa wilaya ya Dar es Salaam kwa kumtusi rais na
kuchochea ghasia baada ya kudai kwamba rais anafikiri kwamba matamshi
yake ni sheria na kwamba siku moja atawaagiza Watanzania kukaa utupu.
Muungano wa mabadiliko na uwazi unaongozwa na Zitto Kabwe ulisema kuwa hatua hiyo ni uendelevu wa utumiaji mbaya wa mamlaka.
''Sheria
inayompatia mkuu huyo wa Wilaya uwezo wa kuagiza kukamatwa kwa mtu,
hailingani na sababu ya kukamatwa kwa bi Mdee'',alisema.
Watu
kadhaa wamekamatwa katika siku za nyuma kwa kuchapisha ujumbe katika
mitandao ya kijamii ambayo mamlaka inadai inaingilia kisiasa.
Mamlaka
inaamini kwamba inafuata sheria na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba
hakuna ''migogoro yoyote miongoni mwa wananchi'' nchini Tanzania.
Bwana
Magufuli alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 na licha ya
kukosolewa na upinzani pamoja na makundi ya wanaharakati anaungwa mkono
na Watanzania wengi.
0 comments:
Post a Comment